Takeshi Edwards
Leo katikapita pita zangu kwenye mtandao wa FACEBOOK, si nikakatiza kwenye page ya jamaa mmoja ambaye anafanya vema katika maswala ya graphics hasa ya zile filamu za kutisha, mpaka sasa ameshafanya filamu nyingi sana na amejizolea mashabiki wengi sana wenye kuutambua mchango na uwezo wake kwenye tasnia, baadhi ya filamu alizozifanya ni ROHO SITA, ONE BY ONE na nyingine ambazo mimi mwenyewe katika pita pita zangu nilitokea kuzipenda filamu hizo...
Kitu ambacho kilinifanya nimuweke hadharani ni kwamba... nilipokuwa napita kwenye picha zake si nikakutana na picha moja inayomuonyesha vizuri sana na kuonyesha jinsi gani alivyohandsome, hii picha watu wengi sana wametupia comment zao lakini kuna jamaa mmoja anayetumia jina la MAJO aliuliza swali hili "sina la kusema kaka lazima unichukulie dada zangu.
Hapa ndipo Takeshi na yeye akatupia neno "Hao tena lazma nichukue kwa kuwa umesema ww brodah!Majo ..
Hapa nikajiuliza kwa nini jamaa aliongea kauli ya kujihami kivile? na je jamaa ameongea kwa uhakika kauli yake ya kuchukua dada za watu?
MAJIBU HAYO MIMI SINA KWASABABU MIMI NILIKUWA NAPITA TU...!
Kama ungependa kusoma na kuona comment nyingine kuhusu picha hiyo bonyeza hapa.