Beka Ibrobzama
Kama kawaida yangu nilikuwa napita katika mtandao wa kijamii FACEBOOK nikakutana uso kwa uso na picha mpya ya kijana Beka Ibrozama msanii wa bongo fleva aliyewahi kutamba na kibao chake cha NATUMAINI (remix).
Siwezi kujiita mmbea lakini nilifanya mawasiliano naye ili kujua nini mipango yake hasa katika muonekano wake maana jinsi anavyoonekana kwenye picha hii mpya sivyo ambavyo alikuwa akionekana wakati wa NATUMAINI, na haya ndiyo yalikuwa maneno yake.
"Hii nikawaida kwangu napenda sana kubadilika, lakini kwa sasa nafurahia sana muonekano huu mpya nilionao na naimani watu wengi wanaotazama picha hii wamekuwa wakinisifia kuwa nimependeza" alisema mkali huyo wa masauti BEKA IBROZAMA.
MIMI NILIKUWA NAPITA TU...
Kama ungependa kutazama picha nyingine za Beka bonyeza hapa
No comments:
Post a Comment