Hapa KISATE akiwa na dogo.
Hivi karibuni nilikuwa mkoani Morogoro nadhani sina sababu ya kuandika nilikwenda kwa nani na kufanya nini, lakini katika pita pita zangu nikapita sehemu kijiji hivi kinaitwa MISONGENI mara ghafla nikakutana na jamaa ambaye nilipomuona tu nikahisi kuwa ninamfahamu, ikanibidi nimsimamishe na kumuuliza maswali kadhaa.
Hapa Kisate akielekeza jambo.
Baada ya maswali yangu matano tu nikawa nimeshamfahamu kumbe ni jamaa ambaye ninamfahamu kabisa na nimekuwa nikipenda sana filamu zake ambazo amekuwa akicheza jina lake anaitwa JACKSON KABIRIGI ambaye watu wengi wanamtambua kama NUNDA kutokana na kukamua vilivyo katika filamu iliyokuwa ikiitwa NUNDA.
Hapa KISATE akiwa na baadhi ya waigizaji.
Sasa bwana nikupashe kitu ambacho kilinishangaza sana moja kati ya maswali yangu ni kutaka kujua ni kwanini nimemkuta katika muonekano ule alionao maana mwanzoni nilidhani kuwa ni chizi fulani hivi kutokana na manguo machafu aliyoyavaa, na haya ndio majibu aliyonipa.
Kutokea kushoto Timoth Conrad, Abdulwakil Kalyuku, Jackson Kabirigi (Kisate)
"Nipo hapa Morogoro wiki ya pili sasa natengeneza filamu yangu mpya itakayoitwa KISATE" alisema Jackson. Na mimi hapo hapo nikapata swali lingine la kumuuliza, nikamuuliza "Je nikwanini ameamua kucheza katika muonekano ule" alichonijibu ni hiki.
"Ni mabadiliko kama ilivyokawaida yangu na safari hii sijabadilika kimavazi tu bali nimebadili mpaka jina kwa sasa ningependa wadau na wapenzi wa filamu zangu waniite KISATE"
Kufikia katika pointi hiyo nikajikuta natamani sana kuona japo sini moja jinsi inavyotengenezwa, ndipo nisubiri mpaka nione.
LAKINI PAMOJA NA YOTE MIMI NILIKUWA NAPITA TU...
Habari zaidi nitakupatia hivi karibuni kuhusu filamu hiyo ambayo inatarajiwa kuwa nzuri kuliko zote alizowahi kucheza.
No comments:
Post a Comment